MKURUGENZi wa habari, uenezi na mahusiano ya umma, kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Mohammed Ngulangwa, amejiuzulu kwa kile alichoita, “kutorodhishwa na mwenendo wa mwenyekiti wake.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …(endelea).
Anasema, “Leo Jumamosi (jana), tarehe 27 Juni 2026, nililazimika kusafiri kutoka Zanzibar kuja kuhudhuria kikao cha Kamati ya Mashauriano kwa upande wa Tanzania Bara, kilichoongozwa na Naibu Katibu Mkuu Bara Mhe. Vedasto Ngombale Mwiru.
“Pamoja na mambo mengine, kikao kiliona ipo haja ya Chama kutoka hadharani kwa ajili ya kukemea tamko haramu la Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobas Katambi, kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya Siasa.
“Kauli hiyo ya Katambi ni kama inatengua kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoitoa mwaka 2024 kwamba kuzuia mikutano ya hadhara ni kuzuia haki ya kikatiba na kisheria kwa vyama vya Siasa,” anaeleza.
Kwa mujibu wake, kikao hicho, kiliamua kufanyike mkutano na waandishi wa habari, leo Jumapili, tarehe 28 Juni, saa 5:00 asubuhi ili kumkumbusha Katambi kwamba hana mamlaka ya kupindua kauli ya Rais, Katiba na sheria.
Hata hivyo, Ngulangwa anasema, “Kwa masikitiko makubwa, baada ya kutoa mwaliko kwa waandishi wa habari na wanachama kuhudhuria mkutano huo, Mwenyekiti wetu, Mirambo Camil Yusuf,!ameagiza kusitishwa kwa shughuli hiyo.”
Anaongeza, “Sababu iliyotolewa, ni kwamba l inaweza kumfanya aonekane hana maana.”
Hivyo basi, Ngulangwa anasema, kuitendea haki nafsi yake, ameamua kujiuzulu nafasi yake ya mkurugenzi wa habari, uenezi na mahusiano ya umma, ili kujipa uhuru wa kusimamia anachokiamini.
“Hivyo, kuanzia leo nitabaki na nafasi yangu ya Ujumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa, Kanda ya Pwani ili kutoa fursa kwa Mhe. Mirambo kuteua Mkurugenzi anayeweza kuendana na mipango yake,” amefafanua Ngulangwa.
CUF – Cham cha Wananchi, kimekuwa kwenye minyukano ya ndani kwa ndani, tangu mwaka 207, baada ya Prof. Ibrahim Lipumba aliyekuwa amejiuzulu wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015, kurejeshwa na serikali kuongoza chama hicho.
Uamuzi huo wa serikali, ulisababisha Maalim Seif Sharif Hamad na viongozi wengine, kuamua kukihama chama hicho na kujiunga na ACT- Wazalendo.
Naye Lipumba aling’olewa na serikali Machi mwaka huu, huku akintuhumu Msajili wa Vyama vya Siasa, Francis Mutungi, kumhujumu.