Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Jamii, CP Alex Mkama
KAMISHNA wa Kamisheni ya Polisi Jamii CP Alex Mkama amewataka wakuu wa Polisi Jamii kuhakikisha wanaongeza juhudi ya kuyafikia makundi yote ndani ya jamii kwa kuhamasisha uhuishaji na uanzishwaji wa vikundi vya ulinzi shirikishi katika mitaa yao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
CP Mkama ametoa rai hiyo alipokutana na wakuu wa Polisi Jamii wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, vikosi na wilaya zake katika makao makuu ya Polisi Jijini Dar es Salaam.
Aidha amewasisitiza pamoja na elimu wanayoendelea kutoa kwa jamii, wahakikishe wanajenga mahusiano na ushirikiano kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto za kiusalama wanazokutana nazo.
Vilevile amewataka kuwaelimisha wananchi kuhusu haki zao ndani ya mfumo wa haki jinai ili kupunguza malalamiko,kwani baadhi ya wananchi wanapata changamoto kwa kutotambua utaratibu.