Clayton Chipando, 'Baba Levo'
MAHAKAMA Kuu Masjala Ndogo ya Kigoma imesogeza mbele usikilizaji wa maombi ya nyongeza ya muda wa kuwasilisha maelezo ya mashahidi wa walalamikaji katika kesi ya uchaguzi wa Jimbo la Kigoma Mjini, kutoka saa 6:00 mpaka saa 8:00 mchana wa leo Alhamis 18 Juni 2026. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kigoma … (endelea).
Kesi hiyo ya uchaguzi namba 28949 ya Mwaka 2025 imefunguliwa na wananchi wanne, Johary Kabourou, Loum Mwitu, Pendo Kombolela na Luma Akilimali dhidi ya Tume Huru ya Uchaguzi, mbunge wa jimbo hilo, Clayton Revocatus Chipando, maarufu Baba Levo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
Walalamikaji hao wanapinga ubunge wa Baba Levo aliyetangazwa kushinda kiti hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, akimzidi mpinzani wake mkubwa kutoka ACT-Wazalendo, mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Zitto Kabwe.