CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinautaarifu umma kuwa tarehe 11 Juni 2026, Mahakama ya Rufani ya Tanzania jijini Dar es Salaam itasikiliza Maombi ya Jinai Na. 7440840/2026 kati ya Jamhuri na Tundu Antiphas Lissu.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Ameyasema hayo Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chama hicho Brenda Rupia amesema kesi hiyo inahusu maombi yaliyowasilishwa katika Mahakama ya Rufani kufuatia mwenendo wa kesi inayomkabili Mwenyekiti huyo wa Chadema, ambapo usikilizwaji wa shauri hilo umepangwa kufanyika kesho katika Mahakama ya Rufani, Dar es Salaam.
Chadema imewahimiza wanachama wake, wafuasi na wananchi wanaopenda kufuatilia mwenendo wa haki na utawala wa sheria kufuatilia kwa karibu usikilizwaji wa shauri hilo, ambalo limevutia mjadala mpana wa kisiasa na kisheria nchini.
Mahakama ya Rufani inatarajiwa kusikiliza hoja za pande zote kuhusu maombi hayo, ambayo yanahusiana na hatua zilizochukuliwa katika kesi ya msingi inayomkabili Tundu Lissu.