MAMLAKA nchini Kenya zimewakamata wanafunzi wanane wa shule ya bweni ya wasichana ya Utumishi Girls Academy wakituhumiwa kuhusika na tukio la moto lililosababisha vifo vya wanafunzi 16 na kujeruhi wengine 79.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Moto huo ulitokea usiku katika bwweni la shule hiyo iliyopo Gilgil, kaunti ya Nakuru. Polisi wanaamini moto huo unaweza kuwa ulisababishwa kwa makusudi, huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo halisi na sababu ya tukio hilo.
Ripoti zinaeleza kuwa baadhi ya milango ya dharura ilikuwa imefungwa wakati moto ulipozuka jambo lililowafanya baadhi ya wanafunzi kushindwa kutoka haraka na wengine kulazimika kuruka madirishani kujiokoa.
Waziri wa Elimu wa Kenya Julius Ogamba amesema walimu wawili walikuwa wamepewa taarifa kuhusu mpango fulani wa wanafunzi lakini hawakuchukua hatua mapema.
Serikali pia imevunja bodi ya shule hiyo huku wazazi wengi wakiendelea kusubiri utambuzi rasmi wa miili ya watoto wao kupitia vipimo vya DNA