ALIYEKUWA Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mchungaji Peter Msigwa ametangza rasmi kurudi katika Chama chake cha zamani cha Chama cha Demokrasia na Maendelea (Chadema) baada ya kuondoka mwishoni mwa mwaka 2024. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa … (endelea).
Mch. Msigwa ametangaza kurudi Chadema kupitia kurasa zake za mitandao kijamii akihusisha matukio ya uvunjwaji wa haki za binadamu zilizotokea wakati wa uchaguzi na baadaya uchaguzi wa Oktoba 29 2025.
Kada huyo aliyewahi kushinda nafasi kadhaa katika Chadema ameandika; “Nimefikiri na kutafakari kwa muda mrefu baada ya matukio ya ukiukwaji wa haki, utu na dhuluma dhidi ya uhai wa binadamu yaliyotokea tarehe 29 Oktoba 2025. Siwezi kuendelea kuishi katika huzuni na ukimya tena.
“Kwa dhamira yangu binafsi, leo nimejiondoa rasmi kutoka CCM na kurejea CHADEMA kwa kufuata taratibu zote za CHADEMA.
“Kwa Watanzania wote, na wanachama wa CHADEMA wale walioumizwa au kukatishwa tamaa na msimamo wangu wa awali, naomba radhi kwa dhati pale nilipokuwa kinyume na matarajio yetu ya pamoja katika safari ya kutafuta haki, utu na demokrasia ya kweli.
“Naam, binadamu hukosea, lakini dhamira inapozinduka ni wajibu kusimama upande unaouona kuwa wa kweli na wa haki.
Asanteni Sana.