UBALOZI wa Marekani nchini Tanzania 21 Mei 2026,umeeleza kuwa Serikali ya Marekani imemuwekea vikwazo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania (SACP) Faustine Jackson Mafwele kwa madai ya kuhusika katika ukiukaji mkubwa wa Haki za Binadamu.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio,marekani imesema inazo taarifa za kuaminika zinazomuhusisha Mafwele na vitendo vya ukandamizaji pamoja na vitendo vya ukiukaji wa Haki za Binadamu.
Aidha Washngton,imesema uamuzi huo umetokana na taarifa za uchunguzi zinazohusiana na matukio ya mwaka 2025,ambapo wanaharakati Agather Atuhaire wa Uganda pamoja na Boniface Mwangi wa Kenya walidai kutekwa,kushikiliwa na kufanyiwa vitendo vya ukatili walipokua Tanzania kufuatilia kesi ya Kiongozi wa Upinzani Tundu Lissu.
Kutokana na hatua hiyo Marekani imesema vikwazo hivyo ni sehemu ya juhudi zake za kuwawajibisha watu wanaotuhumiwa kukandamiza haki za msingi za wananchi ambapo chini ya vikwazo hivyo Mafwele hatoruhusiwa kuingia Marekani.