JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kupatikana kwa David Joseph DJumbe ambaye taarifa zake zilikuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa alikamatwa na watu wasiojulikana katika eneo la Bunju jijini Dar es Salaam.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi, Jeshi hilo lilianza kufuatilia tukio hilo mara baada ya taarifa hizo kusambaa, ambapo katika uchunguzi wa awali walifanikiwa kulipata gari lenye namba T 609 DTD aina ya Toyota Wish rangi nyeusi linalomilikiwa na Allan Elisonguo Macha.
Polisi wamesema gari hilo ndilo ambalo David DJumbe anadaiwa alikuwa akisafiria kama abiria wakati alipokamatwa na watu wanaodaiwa kutokujitambulisha.
Aidha, Jeshi la Polisi limeeleza kuwa David DJumbe tayari amepatikana salama huku uchunguzi zaidi ukiendelea ili kubaini watu waliohusika na tukio hilo pamoja na sababu za kumkamata.
Jeshi hilo limeongeza kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahusika mara baada ya uchunguzi kukamilika.