BIA ya mabingwa kutoka Tanzania, Safari Lager, imeandika historia baada ya kutangaza rasmi udhamini wake wa Kombe la Dunia la FIFA 2026, na kuwa chapa ya kwanza ya bia kutoka Tanzania kupata nafasi kwenye jukwaa kubwa zaidi la soka duniani. Hii ni hatua kubwa inayowahusu mashabiki wote wa soka nchini ambao wameendelea kuamini na kuishi na mchezo huu kwa moyo wao wote. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kwa zaidi ya miaka 40, Safari Lager imeendelea kuwa sehemu muhimu ya maendeleo ya soka Tanzania. Kupitia mashindano ya Safari Cup, programu ya Scout wa Mabingwa pamoja na udhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Safari Lager imekuwa mstari wa mbele katika kukuza vipaji, kuhamasisha ushindani na kuwaunganisha mashabiki wa soka nchini. Udhamini huu wa Kombe la Dunia si jambo la bahati, bali ni matokeo ya safari ndefu ya uwekezaji na imani katika mchezo wa soka.
Udhamini huu mkubwa umebeba pia kampeni mpya ya Safari Lager ijulikanayo kama “Mabingwa Wanastahili.” Kampeni hii imejengwa juu ya ukweli rahisi lakini wenye maana kubwa kuwa si kila mtu hubeba kombe, lakini kila anayejitokeza, anayejitoa kwa moyo wake wote na anayependa mchezo huu kwa dhati ni bingwa.
Kwa mara ya kwanza, chapa ya bia inaweka mashabiki katikati ya simulizi la soka na kuwapa nafasi ya kuthaminiwa kwa mchango wao, mapenzi yao na imani waliyoendelea kuonyesha kwa miaka mingi. Na zawadi hiyo inaanza sasa.
Safari Lager pia imezindua toleo maalum la bia zenye ujazo wa 375mL na 500mL zenye lebo rasmi ya Kombe la Dunia la FIFA 2026, kama ishara ya fahari ya mafanikio haya makubwa. Kila chupa mikononi mwa mashabiki ni sehemu ya historia mpya ya Tanzania kwenye ulimwengu wa soka.
Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Tanzania Breweries Limited (TBL), Khensani Mkhombo amesema:
“Safari Lager siku zote imeamini kuwa mabingwa hawapatikani uwanjani pekee. Ni mashabiki wanaojitokeza kila wakati, wanaouhisi kila mchezo ndani ya mioyo yao na ambao hawajawahi kuacha kuamini. Kwa zaidi ya miaka 40 tumekuwa pamoja nao, na leo tunajivunia kuwapa heshima wanayostahili kwenye jukwaa kubwa zaidi la soka duniani. Hii ni kwa ajili yao.”
Siku ya Jumamosi tarehe 23 Mei 2026, Safari Lager itaendelea kuandika historia kupitia uzinduzi mkubwa utakaofanyika Mwenge, Dar es Salaam. Mashabiki wanahimizwa kufuatilia kurasa rasmi za Safari Lager kwenye mitandao ya kijamii kwa taarifa zaidi kuhusu tukio hilo.
Michuano ya Kombe la Dunia itakapoanza, Safari Lager itaandaa maeneo mbalimbali ya kutazama mechi kote nchini ili kuwaleta mashabiki pamoja na kuwapa burudani, hamasa na uzoefu wa kipekee wa soka.
Kupitia kampeni ya “Mabingwa Wanastahili – Shinda Kibingwa,” mashabiki pia watapata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali. Ili kushiriki, mashabiki wanatakiwa kununua Safari Lager, kuangalia namba ya siri iliyo chini ya kizibo na kuituma kwa SMS kwenda namba 15067 ili kupata nafasi ya kushinda Smart TV au muda wa maongezi papo hapo.
Droo za kila wiki zitaonyeshwa mubashara kila Jumapili saa 11 jioni kupitia TBC1 katika kipindi cha Mabingwa Wanastahili,Shinda Kibingwa. Kadri mshiriki anavyotuma namba nyingi zaidi, ndivyo nafasi yake ya kushinda inavyoongezeka.
Kwa sababu Safari Lager inaamini kuwa Mabingwa Wanastahili.