RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni, anatarajiwa kuapishwa leo Jumanne 12 Mei 2026 kuanza muhula mwingine wa miaka mitano madarakani, hatua itakayoongeza utawala wake kufikisha miaka 45 tangu alipoingia madarakani mwaka 1986.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Sherehe za kuapishwa kwake zitafanyika jijini Kampala na zinatarajiwa kuambatana na gwaride kubwa la kijeshi lililosimamiwa na mtoto wake, Muhoozi Kainerugaba, ambaye pia ni mkuu wa jeshi la Uganda.
Museveni anatajwa kuwa kiongozi wa pili Afrika kwa kukaa muda mrefu madarakani, nyuma ya Paul Biya wa Cameroon ambaye ameiongoza nchi hiyo tangu mwaka 1982.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Afrika akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.