MAKONGORO Nyerere, mtoto wa Baba wa Taifa Julius Nyerere, ameingia katika orodha ya washindi watatu wa droo ya kampeni ya Kombe la Dunia ya benki ya CRDB hatua ambayo imezua mvuto wa kipekee kutokana na historia ya familia yake nchini.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Makongoro alitangazwa mshindi wa safari ya kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia 2026 itakayofanyika Canada, Marekani na Mexico, na baada ya kupigiwa simu kuthibitishiwa ushindi wake alijibu kwa kifupi: “Asante sana.”
Wengine waliobahatika katika droo hiyo ni mfanyabiashara maarufu Arun Lodhia pamoja na Abdulraouf Suleiman, ambao nao wataungana katika safari hiyo ya kihistoria ya kushuhudia Kombe la Dunia.
Katika upande wa zawadi za vifaa vya elektroniki, washindi wa televisheni ni Arina Kaswala, Lusekelo Michael na Easter Kabakama.