RAIS wa Zanzibar Hussein Mwinyi kesho tarehe 09 Mei, 2026 atakuwa mgeni rasmi katika hafla utoaji wa tuzo za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa wanamichezo waliofanya vizuri mwaka 2025 itakayofanyika ukumbi wa The Super Dome, Masaki Jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Tayari Kamati ya maandalizi ya utoaji wa tuzo hizo imejiandaa kikamilifu kufanikisha shughuli hiyo ya kuwaenzi na kuwasherehekea wanamichezo hao waliofanya vizuri kitaifa na kimataifa.
Tuzo mbalimbali 21 zitatolewa ukilinganisha na mwaka 2024 ambapo zilikuwa 20 na kuongezeka tuzo moja ya Mwanahabari Nguli wa Michezo.
Watanzania wanahimizwa kuendelea kupiga kura kuhusu Tuzo ya Mchezaji Bora Chaguo la Watu kupitia WhatssApp (+255-689-525363)