SERIKALI ya Marekani imekataa kutoa viza kwa maafisa sita wa Shirikisho la soka la Senegal, hatua ambayo imezua mjadala nchini Senegal wakati maandalizi ya Kombe la Dunia 2026 yakiendelea.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Kwa mujibu wa Vyombo vya habari vya Senegal, walioathiriwa ni Wanachama wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho akiwemo Amadou Kane, Makamu wa nne wa Rais wa Shirikisho hilo. Mamlaka za Marekani zimesema maombi yao hayakukidhi vigezo kwa sababu mbalimbali, bila kutoa maelezo ya ziada.
Hatua hiyo imekuja wakati ambapo Marekani inaendelea kuongeza ukali wa masharti ya kuingia nchini, licha ya ahadi za FIFA za kurahisisha upatikanaji wa viza kwa wajumbe wanaohusiana na kombe la Dunia.
Nchini Senegal, uamuzi huo umepokelewa kwa hisia tofauti, ambapo baadhi ya wadau wa soka wakiutaja kama fedheha kwa Afrika na changamoto kwa ushiriki wa wadau wa soka katika maandalizi ya mashindano hayo makubwa.