KLABU ya Yanga imetangaza kumfuta kazi Kocha Mkuu, Pedro Goncalves, kufuatia maamuzi ya uongozi wa klabu hiyo na kumkabidhi mikoba Abdihamid Moalin. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo 6 Mei 2026, uongozi wa Yanga umesema umefikia uamuzi huo baada ya tathmini ya ndani,huku ukimshukuru Kocha huyo kwa mchango wake ndani ya timu na kumtakia kila la kheri katika majukumu yake yajayo.
Klabu hiyo imeeleza kuwa timu itakua chini ya makocha Abdihamid Moalin na Patrick Mabedi,watakaoshirikiana kuiongoza timu hiyo hadi mwisho wa msimu.
Hatua hiyo inakuja muda mfupi baada ya Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC.