RAIS wa Kenya, William Ruto amesema kuwa kujengwa kwa kiwanda cha kusafisha mafuta mkoani Tanga nchini Tanzania kutaifanya afrika mzima kupata maendeleo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza leo tarehe 4 Mei 2026 Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Ruto ameeleza kuwa yeye na Rais Samia Suluhu Hassan wamejadili namna mradi huo unatekelezwa Tanga utakavyozifanya nchi za Afrika kunifaika na rasimali zake na kuacha kutegemea mataifa mengine.
Amesema kuwa amezungumza na marais wa mataifa mengine kama vile Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Uganda, Yoweri Museveni.
“Serikali ya Kenya ipo tayari kuwekeza kwenye mradi huu kama ambavyo serikali ya Uganda, Tanzania na Rwanda zilivyokuwa tayari”
“Hii itakuwa fursa kubwa kwa Tanzania kwa kuunda mfumo wa kiuchumi na viwanda,” alisema Rais Ruto.
Amesem kuwa Kenya itakuwa sehemu ya unufaikaji wa haraka kwa sababu ya eneo la Mombasa lipo karibu kwa kilometa 190 kutokea Tanga unapotekelezwa mradi huo.
“Hii itatuwezesha kufanya biashara kubwa pamoja kama jumuiya ya Afrika Mashariki nawaarika wafanyabiashara kuangalia fursa hii.”