KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) imesema kuwa Tume ya Jaji Chande ni batili na imekuwa ni matumizi mabaya ya fedha za umma, Chama hicho kimeeleza kuwa tume hiyo imeficha ukweli huku takwimu zake zikidaiwa kuwa za kutungwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza na waandishi wa habari leo 5 Mei 2026 katika makao makuu ya Chadema yaliyopo Mikocheni, Dar es Salaam, Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Rugemeleza Nshala, amesema tume hiyo imekiuka mipaka ya mamlaka yake kisheria.
Amesema kitendo cha tume hiyo kujihusisha na kutoa amri ya kuchunguza maiti kupitia sheria ya uchunguzi wa vifo ni kinyume cha sheria, kwani haina mamlaka ya kufanya hivyo.
Kwa mujibu wa Nshala, hatua hiyo inaonyesha udhaifu wa kisheria na inaleta mashaka juu ya uhalali wa matokeo ya tume hiyo, huku akisisitiza kuwa Chadema itaendelea kuhoji na kupinga mwenendo wa tume hiyo kwa maslahi ya umma.