BENDERA za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), zitapepea nusu mlingoti kuanzia 29 Oktoba, mwaka huu ili kuwakumbuka watu waliofariki kutokana na matukio yaliyotokea Oktoba 29, 2025.Anaripoti Zakia Nanga Dar es Salaam … (Endelea)
Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, leo tatehe 27 Oktoba 2026, amewaagiza watendaji na viongozi wa chama hicho wapeperushe bendera nusu mlingoti.
Agizo hilo amelitoa jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Mnyika alikuwa akisoma maazimio ya Kamati Kuu ya chama hicho iliyoketi leo, ambapo moja ya maazimio yake ni kupeperusha bendera za chama nusu mlingoti kwa ajili ya kuwakumbuka waliofariki katika matukio hayo.
Akieleza kuhusu agizo hilo, Mnyika amesema: “Bendera za chama zitapepea nusu mlingoti kuanzia 29 Oktoba hadi 4 Novemba”
Hatua hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya kuwakumbuka waliofariki kutokana na matukio ya Oktoba 29, 2025.
Mwisho.