JESHI la Magereza nchini limekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, amegoma kula chakula gerezani na kwamba mawakili wake watatu wamezuiwa kumuona.Anaripoti Zakia Nanga Dar es Salaam … (Endelea)
Akitoa taarifa kwa umma, Msemaji wa Jeshi la Magereza, Elizabeth Mbezi, amesema taarifa hizo si za kweli na zinalenga kupotosha jamii.
Mbezi amesema Lissu yupo salama na hajaanza mgomo wa kula chakula kama inavyodaiwa kwenye mitandao ya kijamii.
Aidha, ameeleza kuwa mawakili wake wanaendelea kumuona kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.
Jeshi la Magereza limewataka wananchi kupuuza taarifa hizo na kuacha kusambaza habari zisizo na ukweli, likionya kuwa kusambaza taarifa za aina hiyo kunaweza kuwa kosa kisheria.
Kauli hiyo ya Magereza imekuja siku nne baada ya mwanasheria mkuu wa Chadema, Dk. Rugemeleza Nshala, kueleza kuwa Lissu angeanza mgomo wa kula chakula kuanzia tarehe 26 Oktoba, 2026.
Mwisho