SERIKALI ya Kenya imesema bado haijapokea taarifa rasmi kutoka kwa taasisi yoyote kuhusu madai ya kutekwa kwa mwanaharakati na mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Twaha Mwaipaya, anayedaiwa kutekwa katika eneo la Kamulu, Kaunti ya Machakos nchini humo.Anaripoti Zakia Nanga Dar es Salaam … (endelea)
Kwa mujibu wa BBC Swahili, Ofisi ya Msemaji wa Serikali ya Kenya, Charles Owino Wahong’o, imesema inaendelea kufuatilia suala hilo licha ya kutokuwa na taarifa rasmi kuhusu tukio hilo.
“Bado hatujapata taarifa kuhusu tukio hilo, hivyo tunalifuatilia,” ilisema taarifa ya ofisi hiyo.
Kwa upande mwingine, gazeti la Mwananchi limeripoti kuwa Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya, kupitia Balozi Dk. Bernard Kibesse, umesema unaendelea kufuatilia taarifa zinazohusu madai hayo.
“Bado taarifa ya tukio hilo hatujazipata, hivyo tunafuatilia,” Dkt. Kibesse amenukuliwa akisema katika taarifa iliyoripotiwa na Mwananchi.
Wakati huo huo, shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International Kenya limeripoti madai ya kutekwa kwa Mwaipaya, likieleza kuwa tukio hilo linadaiwa kutokea tarehe 25 Aprili, 2026.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, watu wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo walitumia magari matatu, likiwamo gari aina ya Toyota Land Cruiser Hardtop.
Hadi sasa, kwa mujibu wa taarifa zilizotajwa, mamlaka za Kenya na Ubalozi wa Tanzania nchini humo zimesema zinaendelea kufuatilia suala hilo.
Mwsho.