GASTON Galubindi, Mkurugenzi wa Sheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amesema kuwa leo, tarehe 26 Oktoba, 2026, huu Mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu, ameanza rasmi mgomo wa kula akiwa gerezani.Anaripoti Faki Sosi, Dar es salaam … (Endelea)
Lissu anayekabiliwa na mashtaka ya Uhaini yupo kwenye Gereza Kuu la Ukonga anakoshikiliwa tangu tarehe 10 Aprili 2025.
Lissu anayesubiri hukumu ya kesi hiyo ametangaza mgomo huo akishinikiza maofisa wa magereza kutofuatilia mazungumzo yake na mawakili wake.
Shinikizo la Lissu linatokana na uamuzi wa Mahakama Kuu, Masjala Kuu ya Dodoma iliyoketi tarehe tarehe 16 Oktoba, mwaka huu kwenye mahakama hiyo Masjala Ndogo ya Dar es Salaam lililotolewa na jopo la majaji watatu likiongozwa na kaimu Jaji Kiongozi Jaji Amir Mruma.
Wakili Galubindi ameiambia MwanaHALISI, kuwa Lissu hajawahi kurudi nyuma kwenye misimamo yake na kwamba hatarudi nyuma mpaka pale gereza la Ukonga litakapofuata amri ya mahakama.
“Mwenyekiti wetu hajawahi kutoa msimamo akayumba ataendelea na msimamo wake kwa gharama yoyote,” amesema Galubindi.
Galubindi amesema kuwa Lissu atabadilisha msimamo wake endapo amri hiyo itakapofuatwa.
Mwisho
