KANISA Katoliki nchini limetangaza kuwa tarehe 29 Oktoba, mwaka huu litafanya ibada maalumu ya kuwaombea waliouawa na kujeruhiwa katika ghasia za Oktoba 29 mwaka jana.Anaripoti mwandishi wetu, Dar es salaam …. (Endelea)
Wito huo umetolewa leo tarehe 23 Oktoba, 2026 na Wolfgang Pisa, Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa hilo (TEC), kupitia barua iliyokwenda kwenye kila lilipo kanisa hilo nchi nzima.
“Kwa moyo wa kiuchungaji na kwa kutambua wajibu wetu wa kuliongoza taifa la Mungu, katika ukweli, haki, upendo na mwanga wa Injili.
“Kwa barua hii nawaalika kuadhimisha misa takatifu kwa ajili ya kuliombea taifa letu Tanzania na sisi wenyewe. Katika kutimiza mwaka mmoja tangu uchaguzi wa mwaka jana,”.
Tunakumbuka baadhi ya watu wetu kuumizwa, kupotea na hata kuuawa, hali hiyo ya maumivu na msiba bado ipo kati ya watu wetu,”.
Katika mazingira hayo tunaitwa kusimama pamoja kama jumuiya ya waumini tukimkabidhi Mungu mwenye huruma na taifa letu…tukiomba umoja, upendo, ukweli mshikamano ambavyo ni matunda ya haki,” .
Barua hiyo imeeleza kuwa misa hiyo ifanyike siku ya Alhamisi tarehe 29 Oktoba, mwaka huu kwenye parokia, vituo vya sala na taasisi za kanisa kadri iwezekanavyo.
Mwisho.