ANANILEA Nkya, Mchambuzi wa masuala ya siasa nchini ametaka viongozi wa serikali waliokuwepo wakati wa ghasia zilizopelekea mauaji ya Oktoba 29 wajiuzulu na kuwajibika.Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Ametoa mfano wa uwajibikaji serikalini ambapo mwaka 1977 Ali Hassan Mwinyi, akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani alijiuzulu kwa mauaji ya watu wasiokuwa na hatia.
Ameongeza kuwa tarehe 22 Januari 1977 Mwinyi alilazimika kuchukua hatua hiyo baada kutokea mauaji ya watu wasio na hatia na operesheni dhidi ya vikongwe (washukiwa wa uchawi) katika mikoa ya Mwanza na Shinyanga (Kanda ya Ziwa).
Nkya anasema mauaji yaliyojitokeza Oktoba 29 yalipaswa kuwa sababu kwa serikali kujiwajibisha.
Mwisho.