MAHAKAMA Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam imetupilia mbali ombi la Said Issa Mohammed na mwenzake la kutaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuzuiwe kufanya shughuli zake.Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Uamuzi huo umetolewa leo tarehe 22 Oktoba 2026, na Jaji Awamu Mbagwa.
Maombi hayo ni maombi madogo kwenye shauri la msingi la Saidi Issa na mwenzake Hamad Khamis Rashid la kuiomba Mahakama Kuu kukichukulia hatua Chadema kwa kudai hakitoi mgawanyo wa mali ulio sawa upande wa Zanzibar.
Awali tarehe 28 Mei 2026 Mahakama Kuu ilitupilia mbali kesi kama hiyo iliyofunguliwa na Said Issa , Rashid na Maulida Anna Komu (Marehemu) likiwa na madai hayo hayo.
Uamuzi huo una maana kwamba Chadema kitaendelea kufanya shughuli zake ikiwa shauri la msingi likiendelea.
Mwisho.