MWANASHERIA Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Lugemeleza Nshala, amesema maombi ya Said Issa Mohammed ya kutaka Chama hicho kiwekewe zuio la kufanya shughuli za siasa yametupiliwa mbali kutokana na maombi yake kutothibitisha vigezo vinavyohitajika ili kuwekwa kwa amri ya zuio hilo.Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Dk. Nshala ameeleza hayo leo 22 Oktoba 2026 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam ambapo
Amesea Mahakama Kuu imekataa vigezo hivyo na kwamba iliona Said Issa na wenzake walithibitisha kigenzo kimoja pekee lakini vingine viwili walishindwa kuvithibitisha.
“Mahakama Kuu imekataa katika vile vigezo vitatu, vya kutoa amri ya zuio imeona wamethibitisha kimoja lakini vile viwili wameshindwa kuvithibitisha, na kwa maana hiyo jaji akaamua kwamba atupilie mbali maombi yao”. Amesema Dk. Nshala.
https://youtu.be/-RgDShDgaqE
Mwisho.