MAHAKAMA Kuu ya Dodoma iliyoketi Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imetoa amri kwa maofisa wa magereza na Mkuu wa Gereza la Ukonga kutosikiliza mazungumzo ya Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), na Mawakili.Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Lissu anayeshikiliwa kwenye Gereza Kuu la Ukonga tangu tarehe 10 Aprili 2025 akikabiliwa na mashtaka ya uhaini. Na kwamba shauri hilo limeshasikilizwa na kwamba zimesalia siku 23 za mahakama hiyo kutoa hukumu kwenye kesi ya uhaini ambapo tarehe 6 Novemba itakuwa ndio siku ya hukumu hiyo.
Lissu amekuwa akilalamika maofisa wa gereza hilo kusikiliza mazungumzo yake na mawakili wake jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Katika shauri la kikatiba Na. 7300 la Mwaka 2026 lililofunguliwa na Mawakili wa Lissu Mahakama hiyo imesema kuwa Mkuu wa gereza hilo na maofisa wake wamekwenda kinyume na kanuni ya 13 ya kuendesha magereza.
​Uamuzi huo umetolewa leo tarehe 16 Oktoba 2026 na jopo la Majaji watatu wanaosikiliza shauri hilo, linaloongozwa na Kaimu Jaji Kiongozi Amir Mruma, akisaidiwa na Jaji Dk. Angelo Rumisha pamoja na Jaji Dk. Evaristo Longopa.
​Shauri hilo la kikatiba lilifunguliwa na mawakili wa Lissu akiwemo William Maduhu, Nashon Nkungu, na Paul Kisabo wakilalamikia kuwekewa vizingiti vya kuonana na mteja wao gerezani pamoja na kuingiliwa kwa faragha ya mawasiliano na mashauriano yao ya kisheria.
*Mwisho*
​