MSHTAKIWA wa kesi ya uhaini Tundu Lissu ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kesho tarehe 11 Agosti 2026, ataendelea kumuhoji maswali ya Dodoso shahidi wa 16 wa Jahmuri. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Shauri hilo liliendelea leo tarehe 10 Agosti 2026 kwenye mahakama Kuu masjala ndogo ya Dar es Salaam mara baada ya kusimama kwa miezi mitano.
Kesi hiyo iliendelea kwa kwa Jamhuri kuleta shahidi wa 16 ambaye ni ACP Amin Mahamba, anayefanya kazi kwenye moja ya vitengo ofisi ya mpelelezi wa makosa ya jinai (DCI) Dar es Salaam.
ACP Mahamba alitoa ushahidi wake akiongozwa na wakili Mkuu wa Serikali Nassoro Katuga ambapo pamoja na mambo mengine alielezea Mahakama kuwa matamshi ya Lissu yalikuwa na lengo la kuitishia Serikali.
Mara baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake Lissu alianza kumuuliza shahidi huyo maswali ya awali ya dodoso na kueleza Mahakama kuwa kesho ataendelea kumuuliza shahidi huyo maswali katika maeneo 54 ambayo anaona yana mapungufu kwenye ushahidi wake.