SHAURI la kikatiba lililofunguliwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu ya Dodoma, na Mawakili wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @chadematzofficial Tundu Lissu wakilalamikia kunyimwa kumuona gerezani na kukosa faragha pindi wanapomuona linaendelea muda huu katika kikao kinachoketi katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Leo 22 Julai 2026 Mkuu wa Gereza la Ukonga atahojiwa maswali ya dodoso kama shahidi upande wa wajibu maombi ambapo shauri hili la kikatiba na 7300/2026 limefunguliwa na Mawakili Kulwa Maduhu, Nashon Nkungu na Paul Kisabo na lipo mbele ya Jopo la Majaji watatu Amir Mruma, Dk. Angelo Rumisha na Dk. Evaristo Longopa.
Wajibu maombi katika shauri hili ni Afisa Inchaji wa Gereza Ukonga (Mkuu wa Gereza), Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tundu Lissu na chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS).