CHAMA cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kwa kushirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na mwanasiasa maarufu, Dk Willbrod Slaa, wamefungua kesi ya kikatiba dhidi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi na wenzake sita. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
TLS na wenzake wamefungua kesi hiyo Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Tabora, chini ya hati ya dharura wakipinga kauli aliyoitoa bungeni hivi karibuni kuhusiana na zuio la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.
Mbali na Katambi, aliyeshtakiwa kwa jina lake, wadaiwa wengine katika kesi hiyo ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
Pia, wamewaunganisha wadhamini waliosajiliwa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na wadhamini waliosajiliwa wa chama cha ACT- Wazalendo.
Tarehe 26 Juni 2026, akiwa bungeni jijini Dodoma wakati vikao vya Bunge vikiendelea, Waziri katambi alipiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa nchini kote kwa kile alichoeleza ni sababu za kiusalama, akamuelekeza IGP kutekeleza agizo hilo.