Tundu Lissu akiwa mahakamani
KATIBU Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, ameitaka Mahakama ya Rufani Tanzania kuhakikisha inatenda haki kwa usawa katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza na MwanaHALISI Digital leo katika ofisi zake zilizopo Ilala Boma, jijini Dar es Salaam, Sheikh Ponda alisema ni muhimu vyombo vya utoaji haki vikazingatia misingi ya haki na usawa bila upendeleo, ili kulinda imani ya wananchi katika mfumo wa sheria.
Alisisitiza kuwa kila mtu anayefikishwa mbele ya vyombo vya sheria anapaswa kupewa haki zake kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi, bila kujali nafasi yake kisiasa au kijamii.
Kauli hiyo imekuja wakati kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu ikiendelea kuvutia mjadala mpana miongoni mwa wadau wa siasa, sheria na haki nchini.
Kwa mahojiano kamili ya Sheikh Ponda Issa Ponda, tembelea ukurasa wa YouTube wa MwanaHALISI TV pamoja na kurasa zetu nyingine za mitandao ya kijamii.