Sheikh Ponda Issa Ponda
KATIBU wa Shura ya Maimamu Tanzania na mwanasiasa, Sheikh Ponda Issa Ponda amesema hali ya kisiasa nchini Tanzania ni ngumu kutokana na kile alichodai kuwa ni udhaifu mkubwa wa mifumo ya kisheria, akieleza kuwa mifumo hiyo ni kandamizi na inazuia kujengwa kwa mazingira bora ya kisiasa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza kuhusu hali ya kisiasa nchini, Sheikh Ponda alidai kuwa endapo mifumo hiyo haitabadilishwa, Watanzania hawapaswi kutarajia kufanyika kwa uchaguzi huru na wa haki.
“Bila mabadiliko ya mifumo ya Kisheria,watanzania tusahau uchaguzi huru na wa haki ni kitu ambacho hakiwezekani”.Alisema Sheikh Ponda
Sheikh Ponda Amesisitiza kuwa hali ya kisiasa itaendelea kuwa ngumu zaidi ikiwa hakutakuwa na mabadiliko ya mifumo iliyopo.
Aidha, Sheikh Ponda alisema tatizo jingine ni kwamba viongozi hawana dhamira ya kweli ya kufanya mazungumzo ya kisiasa,kwa mujibu wake, badala ya kutafuta suluhu kupitia mazungumzo, viongozi wanatumia vyombo vya dola kudhibiti wananchi.