MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Kigoma leo Alhamisi tarehe 16 Julai 2026, Mahakama imeifuta kesi ya uchaguzi iliyokuwa imefunguliwa Mahakamani hapo na wananchi wanne (4) waliojitambulisha kuwa wapiga kura wa Jimbo la Kigoma Mjini dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini (CCM) Clayton Revocatus Chipando (Baba Levo). Anaripoti Mwandishi Wetu, Kigoma … (endelea).
Uamuzi uliosomwa Mahakamani hapo leo na Jaji Victoria Nongwa aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo iliyokuwa inapinga uhalali wa ‘Ubunge wa Baba Levo’ amesema hoja zote zilizoletwa na walalamikaji ikiwemo hoja za utekaji, madai ya rushwa, udini zimeshindwa kuishawishi Mahakama moja kwa moja kukubaliana kutokana na kwamba ushahidi uliowasilishwa Mahakamani hapo umekosa mashiko
Mahakama imesema kutokana na dosari kadhaa zilizobainishwa na Mahakama kutoka kwa walalamikaji ambao ni wanachama wa ACT Wazalendo, ushahidi uliowasilishwa Mahakamani hapo haina mashiko na kwamba walalamikiwa wote ikiwemo INEC hawana kesi ya kujibu