KAMATI tendaji ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Pemba imemvua uanachama aliyekuwa Makamo Mwenyekiti wa cham hicho visiwani Zanzibar, Saidi Issa Mohammed kwa tuhuma kuiuka Katiba na miongozo ya chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Pemba … (endelea).
Abdullah Hassan Katibu wa Chadema, Kanda hiyo kupitia taarifa yake ya umma amesema kuwa kamati hiyo imeketi jana tarehe 6 Juni 2026, kwenye ukumbi wa Pride ulikuwepo Chakechake visiwani humo.
Hassan amesema kuwa kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa kanda hiyo, Omar Nassor kilijadili mwenendo wa Said Issa na kubaini kuwa ni kinyume na chama hicho.
“Tunautaarifu umma kuanzia jana tarehe 6 Juni Saidi Issa Mohammed si mwanachama na wala hatambuliki kama kiongozi au mwakilishi wa chama katika ngazi yoyote.
“Hivyo kauli, matendo au shughuli zozote atakozozifanya baada ya tarehe hiyo zitakuwa ni za kwake binafsi na hazitahusishw na chama.