LUHAGA Joelson Mpina, aliyekuwa mgombea urais wa chama cha ACT-Wazalendo, amedai kuwa upinzani wa kisiasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ndio chanzo cha vurugu za 29 Oktoba. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Amesema, “Kuna eneo muhimu ambalo Tume ya Jaji Chande (Mohammed Othuman Chande), imelitaja kuwa chanzo cha vurugu za 29 Oktoba mwaka jana. Kwamba, vurugu zile zimetokana na serikali kutotenda haki. Haya mambo yalikuwa yanafichwa na watawala, nashukuru Mungu Jaji Chande ameyaanika.”
Alitoa kauli hiyo, wakati akizungumza na waandishi wa habari, katika ukumbi wa Msimbazi Center, jijini Dar es Salaam, leo Jumatatu, tarehe 1 Juni 2026.
Alisema, “Mwisho wa ubaya aibu. Ripoti ya Jaji Chande, imethibitisha kwamba vurugu zilizotokea kwenye uchaguzi mkuu wa 29 Oktoba, zimesababisha na utapeli wa kisiasa wa Chama Cha Mapinduzi na kushindwa kuwajibika.”
Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV.