Said Issa Mohammed
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam leo tarehe 28 Mei 2026, Mahakama imeifuta rasmi na kuindoa Mahakamani Hati ya kesi Na. 8323/2025 ya madai iliyofunguliwa na Said Issa Mohammed, aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar na wenzake dhidi ya bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), iliyokuwa inahusu usawa kwenye mgawanyo wa mali za chama hicho kati ya Tanzania Bara na Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Katika uamuzi wake uliotolewa muda mfupi uliopita mahakamani hapo kupitia kwa Jaji David Ngunyale, imeeleza kuwa wadai (waliofungua kesi) hawakuonesha -kifungu chochote kwenye hati ya madai kinachoonesha kwamba uvunjifu huo (unaolalamikiwa na wadai) ulianza lini, jambo lililopelekea mahakama kushindwa kujiridhisha kama ina mamlaka au la ya kuendelea kusikiliza kesi hiyo
Jaji Ngunyale amesema hati ya madai ilikuwa ina mapungufu makubwa, hivyo pingamizi lililowekwa na Chadema lina msingi.