Watoto wanaolelewa katika kituo cha UMRA Children Center Magomeni wamepata sababu ya kutabasamu baada ya Meridianbet kutoa msaada wa vyakula kupitia programu zake za Uwajibikaji kwa Jamii.
Msaada huo umehusisha vyakula na bidhaa mbalimbali muhimu ikiwemo mchele, unga, mafuta ya kupikia, sukari pamoja na mahitaji mengine yanayotumika kila siku katika kituo hicho.
Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya MERIDIANBET au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Akizungumza wakati wa utoaji wa msaada huo, mwakilishi wa Meridianbet, Nancy Ingram alisema kampuni hiyo itaendelea kutumia nafasi yake kusaidia jamii na kugusa maisha ya watu wenye uhitaji nchini Tanzania.
“Kila tunapopata nafasi ya kusaidia jamii tunaiona kama sehemu ya wajibu wetu. Watoto hawa ni sehemu ya taifa letu na wanahitaji upendo pamoja na msaada wa karibu,” alisema.

Uongozi wa UMRA Children Center umeishukuru Meridianbet Tanzania kwa msaada huo huku ukisema kuwa mchango huo utasaidia kuboresha maisha ya watoto hao na kupunguza changamoto za mahitaji ya kila siku.