Rais wa TLS, Boniface Mwabukusi
RAIS wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi, amesema Tanzania inapaswa kujifunza kusema ukweli, akisisitiza kuwa kufanya hivyo ni sehemu ya uwajibikaji na msingi wa kurejesha matumaini kwa wananchi.Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Mwabukusi ameyasema hayo leo 7 Oktoba 2026, jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa Uongozi Mpya na Nembo ya Baraza la Vyama vya Siasa.
Amesema katika uwanja wa siasa, viongozi na wadau wanapaswa kuwa na ujasiri wa kusema ukweli kuhusu mambo yanayohusu taifa, badala ya kuficha hali halisi.
“Kwenye taifa hapa tulipo ni lazima tujifunze kusema ukweli, kwa sababu tukisema ukweli ni dalili ya kuwajibika. Kwa sababu ukisema ukweli ndiyo inaweza kurejesha matumaini kwa watu. Kwenye uwanja wa siasa tujifunze kusema ukweli,” amesema Mwabukusi.
Amesema kusema ukweli kuna nafasi muhimu katika kujenga upya imani ya wananchi na kurejesha matumaini katika mifumo ya kisiasa na uongozi wa nchi.