KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) imesema kuwa Tume za uchunguzi wa matukio ya ‘Oktoba 29’ hazina uhalali kwa kuwa uundwaji wake upo kinyume cha sheria.Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Akisoma maadhimio ya kikao cha Kamati kuu ya chama hicho kilichofanyika tarehe 29 Agosti 2026, Dk. Rugemeleza Nshala, Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amesema kuwa uundwaji wa tume hiyo umekinzana na sheria ya tume za uchunguzi nchini sura Na.32, kifungu cha 3 (1).
Dk. Nshala amesema kuwa tume hiyo imekosa uhalali kwa kuwa Muundaji ni sehemu ya walalamikiwa.