Mchezo wa raundi ya nne ya Championship utachezwa leo Jumatano, Septemba 2, 2026, saa 22:00 usiku, katika uwanja wa Turf Moor, mjini Burnley. Hii itakuwa mara ya kwanza timu hizi kukutana tangu walipotoka sare bila mabao Desemba mwaka jana, na sasa zote mbili zinatafuta kujijenga upya baada ya misimu yenye mchanganyiko wa matokeo.
Burnley iliyokuwa mojawapo ya timu bora zaidi za Championship chini ya makocha Vincent Kompany na Scott Parker huko nyuma kabla ya kupanda Ligi Kuu, imerejea daraja la pili baada ya kushuka kutoka Premier League.
Chini ya kocha Nicky Hayen, mwanzo wao wa msimu huu haujawa rahisi walitolewa kwenye EFL Cup na Notts County kupitia mikwaju ya penalti baada ya sare ya 1-1, kisha wakafanikiwa kutoka sare dhidi ya West Ham United baada ya kuwa nyuma mabao 0-2 nyumbani. Hata hivyo, hivi karibuni walifungwa dhidi ya West Bromwich Albion na Norwich City, ingawa bado wanashikilia nafasi ya tano katika msimamo.
Middlesbrough ilimaliza msimu katika nafasi ya tano msimu uliopita, lakini iliangushwa katika mchujo wa kupanda daraja (play-off) na Southampton, kisha ikapoteza tena nafasi yao ya kupanda kwa Hull City baada ya Southampton kuondolewa kwa makosa ya kiutawala.
Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Msimu huu Middlesbrough wanashikilia nafasi ya kumi katika msimamo, wakijaribu kujenga msimamo imara zaidi baada ya msukosuko wa msimu uliopita ambao ulizima ndoto zao za kupanda Ligi Kuu.
Kihistoria, mechi kati ya Burnley na Middlesbrough zimekuwa na ushindani mkubwa, huku takwimu za awali zikionyesha ushindi sita kwa kila upande na sare nne katika michezo ya hivi karibuni.
Mchezo wao wa mwisho, uliokuwa sare bila mabao, unaonyesha ni jinsi gani timu hizi mbili zinavyoweza kuzuiana kwa urahisi zinapokutana, jambo linalofanya mechi hii kuwa ngumu kutabiri.
Kwa kuzingatia hali ya sasa ya Burnley wakiwa juu zaidi katika msimamo licha ya matokeo mabaya ya hivi karibuni, na Middlesbrough wakijaribu kurejesha kujiamini baada ya kukosa kupanda daraja msimu uliopita, mechi hii inatarajiwa kuwa na ushindani mkali.