MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Emmanuel Nchimbi ameeleza kuwa anatamani kumtambua mwanaharakati yeyote kwa uwezo wake wa kufikiri na kushawishi akisisitiza kuwa anatamani pia kujenga taifa ambalo watu wenye mitazamo tofauti wanaweza kukaa pamoja na kuzungumza mambo ya nchi yao kwa amani, bila kuwepo kwa uhasama au uadui.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Nchimbi ameeleza matamanio hayo akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) unaofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, leo 24 Julai 2026.
Aidha, ametoa wito kwa kila Mtanzania kutumia nafasi aliyonayo kurudisha umoja na mshikamano, pamoja na kusimamia haki kama msingi wa amani.