WAKILI Peter Madeleka amesema kuwa uanaharakati hauhusiani na vitendo vya ugaidi, akisisitiza kuwa mtu anayefanya kosa la ugaidi anapaswa kuwajibika kwa mujibu wa sheria kama ilivyo kwa makosa mengine ya jinai.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Madeleka amesema kuwa kuwa mwanaharakati hakumfanyi mtu kuwa gaidi, akieleza kuwa kila tuhuma ya jinai inapaswa kuchunguzwa na kuamuliwa kwa kuzingatia ushahidi na sheria husika, badala ya kuhusishwa na shughuli halali za uanaharakati.
Amesisitiza umuhimu wa kutenganisha uanaharakati na vitendo vya uhalifu, akibainisha kuwa wanaharakati wana nafasi muhimu katika jamii kwa kutetea haki, kuhamasisha uwajibikaji na kuibua hoja zinazohusu maslahi ya wananchi.
Kauli hiyo imekuja wakati kukiwa na mjadala kuhusu nafasi ya uanaharakati na namna unavyotazamwa katika jamii, huku Madeleka akisisitiza kuwa kila mtu anayefanya kosa anapaswa kuwajibika kwa matendo yake binafsi bila kuhusisha hadhi au shughuli anazozifanya.