BAADHI ya waendesha bajaji katika Manispaa ya Lindi wamegoma kufanya kazi leo 22 Juni 2026, wakipinga utozwaji wa faini zinazotokana na makosa ya usalama barabarani.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Waendesha bajaji hao wanadai kuwa wamekuwa wakitozwa faini mara kwa mara, hususan kutokana na kosa la kubeba abiria zaidi ya idadi inayoruhusiwa kisheria.Mgomo huo ulianza mapema asubuhi na kuathiri shughuli za usafiri katika maeneo mbalimbali ya manispaa hiyo.
Tayari Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Lindi amewasili eneo husika kwa ajili ya kufanya mazungumzo na waendesha bajaji hao ili kutafuta suluhisho la mzozo huo.
MwanaHALISI Digital itaendelea kukuletea taarifa zaidi kadri zitakavyokuwa zinapatikana kupitia majukwaa yake ya kijamii.