Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeunda kamati maalum ya Katiba mpya, itakayohakikisha katiba mpya inapatikana kabla ya 2027.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Akizungumza na waandishi habari leo tarehe 17 Juni 2026, John Mnyika Katibu Mkuu wa chama hicho amesema kuwa kamati kuu imeunda Kamati hiyo yenye wajumbe 11 itakayoongozwa na Mwenyekiti wake Dk. Rugemeleza Nshala.
Mnyika amesema Katibu wa Kamati hiyo ni Wakili Deogratius Mahinyila (Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema Bavicha).
Wajumbe wengine ni pamoja na; Wakili Ali Ibrahim, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Suzan Lymo, Ruth Mollel, Pamela Maassay, Wakili Gaston Galubind, Zeud Mvano, Boniface Jacob.
Na wajumbe wawili washauri wa Kamati ambao ni Wakili Mpale Mpoki, na Wakili Jeremiah Mtobesya, ambao si wanachama wa Chadema wameteuliwa kama washauri.
Kamati hiyo itakuwa na hadidu rejea nne ikiwemo kuandaa mkakati wa kukwamua mchako wa Katiba mpya, kuanda rasimu ya muswada wa sheria ya Katiba mpya kwa niaba ya Wananchi utakaolekeza utaratibu wakukwamua mchakato wa Katiba mpya, kuandaa mapendekezo juu ya muuondo na chombo huru kitachosimamia kura ya maoni ya Katiba mpya , na kuzingatia katika ratiba mapendekezo yote yawezeshe mchakato wa Katiba mpya kuanza mapema na sio zaidi ya mwaka 2027.