MWANASIASA na aliyekuwa Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, amesema kujiunga kwake na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ilikuwa ni hatua ya makosa na ameomba radhi kwa wale walioathiriwa na uamuzi huo.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Msigwa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Medani za Siasa kinachoendeshwa na mtangazaji Chief Odemba, ambapo pia alieleza kuwa tangu alipoondoka Chadema hajawahi kukutana na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.
Aidha, Msigwa alisema kurejea kwake Chadema hakulengi kuanzisha migogoro ndani ya chama, bali kushiriki katika juhudi za kukijenga na kukiimarisha.
Alisisitiza kuwa kipindi cha uchaguzi kimekwisha na sasa ni wakati wa wanachama kuweka tofauti zao pembeni na kuelekeza nguvu katika kuimarisha chama.
“Nilikosea kwenda CCM ndiyo maana naomba radhi. Sijarudi Chadema kuleta migogoro, mambo ya uchaguzi yamekwisha, sasa tujenge chama chetu,” alisema Msigwa.