NI mchezo wa kwanza wa mchezo wa kuamua timu itakayocheza Ligue 1 msimu ujao, na unapigwa leo Mei 26, 2026 saa 21:45 kwenye uwanja wa Stade Geoffroy Guichard.
Saint Etienne wana nafasi ya kurejea Ligue 1 baada ya kumaliza nafasi ya tatu Ligue 2 na kufuzu kupitia ushindi wa penalti dhidi ya Rodez. Nice wana jukumu la kujiokoa kwenye Ligue 1 baada ya kumaliza nafasi ya 16, na mechi ya pili itapigwa Mei 29 nyumbani kwao Allianz Riviera.
Wanaingia mechi hii wakiwa na morali safi baada ya kushinda penalti dhidi ya Rodez, ingawa katika michezo yao minne ya mwisho ya ligi wamefungwa mara tatu. Wachezaji hatari ni pamoja na Ibrahim Sissoko mshambuliaji mwenda kasi na Mathieu Cafaro kiungo mwenye uwezo wa kupiga pasi za hatari na mipira ya adhabu. Safu ya ulinzi inaongozwa na Mickael Nade na Dennis Appiah. Kipa Etienne Green anaweza kuanza baada ya kuwa muhimu kwenye mfululizo wa penalti.
Nice wana changamoto kubwa kisaikolojia baada ya kupoteza Fainali ya Coupe de France kwa Lens kwa 3-1, na hawajashinda katika michezo mitano mfululizo. Nahodha wao Dante (umri 42) ndiye tegemeo la safu ya ulinzi, akiwa na uzoefu wa kucheza Ligi ya Mabingwa. Wengine wanaotarajiwa kuleta tofauti ni Gaetan Laborde mshambuliaji, Jeremie Boga winga mwenda kasi, na kipa Yehvann Diouf ambaye anaweza kuwa muhimu kuzuia mashambulizi ya wapinzani.
Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Takwimu zinaonyesha kuwa Nice wamekuwa wakitawala katika mechi za hivi karibuni, wakishinda mechi zote tano za mwisho dhidi ya Saint Etienne ikiwemo ushindi wa 2-1 Coupe de France Desemba 2025 na ushindi wa kihistoria wa 8-0 mwaka 2024.
Saint Etienne wanatarajiwa kutumia mkakati wa kukaba kwa nguvu mapema na kutumia mashambulizi ya pembeni, wakati Nice watapendelea kusubiri na kukera kwa kasi ya Laborde na Boga. Nice watazuiwa kucheza na mashabiki kwenye mechi ya pili Mei 29 kwa sababu ya adhabu ya mashabiki wao.
Licha ya Nice kuwa na ubora wa wachezji na historia ya ushindi, wanaingia mechi wakiwa na kiwango cha chini sana. Saint Etienne wanachukua nafasi ya nyumbani na wana morali safi baada ya kufuzu kwa penalti. Hivyo, mechi ya leo inaweza kuisha kwa sare au ushindi wa mabao 2-1 kwa Saint Etienne. Kwa Nice, lengo ni kuepusha kufungwa kwa tofauti kubwa na kuhifadhi nafasi kwa mechi ya pili nyumbani Mei 29, ambapo watakuwa na wachezji wao wote wa kimataifa nyuma yao.