SERIKALI ya Uganda imeahirisha maadhimisho ya kila mwaka ya Siku ya Mashahidi yaliyokuwa yafanyike 3 Juni kufuatia hofu ya kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola kutoka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya mashauriano kati ya Serikali, kikosi kazi cha kitaifa cha kukabiliana na majanga pamoja na viongozi wa dini.
Museveni amesema hatua hiyo imelenga kuzuia hatari ya maambukizi ya Ebola, hasa wakati ambapo maadhimisho hayo huvutia maelfu ya mahujaji kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika Mashariki.
Taarifa zinaeleza kuwa tayari idadi kubwa ya mahujaji waliokuwa wakitembea kwa miguu kutoka Jimbo Katoliki la Butembo-Beni mashariki mwa DRC, eneo lililoathiriwa na mlipuko wa sasa wa Ebola, waliingia Uganda 15 Mei na kwa sasa wapo Wilaya ya Kasese.
Serikali ya Uganda imeendelea kusisitiza tahadhari na ufuatiliaji wa karibu wa hali ya afya mpakani ili kudhibiti uwezekano wa kuenea kwa ugonjwa huo.