RAIS wa Tanganyika Law Society (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, ameitaka Serikali kuhakikisha mchakato wa maridhiano nchini unaanza kwa kuzingatia ukweli, uwazi na uwajibikaji ili kurejesha imani kwa wananchi.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Akizungumza kuhusu hali ya nchi na matukio mbalimbali yaliyoibua mjadala mkubwa katika jamii, Mwabukusi alisema kuna mambo yanayotokea ambayo si ya kawaida na hayapaswi kufumbiwa macho.
“Maiti kupotea mochwari sio kitu cha kawaida, watu kutandikwa risasi wakiwa majumbani mwao sio kitu cha kawaida. Kwenye suala hili haihitajiki kufunika kombe mwanaharamu apite, kwenye suala kama hili huwezi kufunika,” alisema Wakili Mwabukusi.
Amesisitiza kuwa ili maridhiano yawe na maana na kuleta matokeo chanya, ni lazima kuwe na uwajibikaji kwa matukio yote yanayolalamikiwa na wananchi pamoja na hatua za wazi kutoka kwa mamlaka husika.