SPIKA wa Bunge la Uganda Anita Among ametangaza rasmi kujiondoa katika kinyang’anyiro cha Uspika wa Bunge kwa muhula wa 2026–2031.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Katika taarifa yake, Among alisema amefikia uamuzi huo baada ya kufanya mashauriano ya kina na viongozi wa chama pamoja na wadau mbalimbali wa kisiasa, Amesema hatua hiyo inalenga kuweka mbele umoja wa chama na maslahi ya taifa kuliko maslahi binafsi ya kisiasa.
Among, alieleza kuwa ataendelea kulitumikia taifa katika nafasi nyingine atakayopewa na chama chake pamoja na serikali.Aidha, aliwashukuru Wabunge, Viongozi na Wananchi waliomuunga mkono katika kipindi chake cha Uongozi.
Tangazo hilo limezua mjadala mkubwa katika duru za kisiasa nchini Uganda, huku wachambuzi wakisema huenda likaathiri mwelekeo wa uchaguzi wa Viongozi wa Bunge katika muhula ujao wa 2026–2031.