MKUU wa Wilaya ya Kilindi Mkoa wa Tanga, Fauzia Ngatimbura,amesema kuwa kazi kubwa atakayoanza nayo katika Wilaya hiyo ni kupambana na migogoro ya ardhi iliyodumu kwa muda mrefu.Anaripoti Danson Kaijage,Kilindi … (endelea)
Ahadi hiyo ameitoa kutokana na malalamiko ya migogoro ya ardhi ya wananchi wa Kijiji cha Kwekinkwembe ambao baadhi wametishia kijivua unachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na vyama vya upinzani.
Fauzia amesema kuwa licha ya kwamba ameingia ofisini siku chache zilizopita lakini atahakikisha anafanya kazi za wananchi kadri ya uwezo wake.
“Siwezi kuongelea zaidi juu ya migogoro ya ardhi kwa sasa ila najua kuwa migogoro ipo na kama unavyojua mimi ndio nimeingia ofisini siku mbili zilizopita.”
“Naelewa kuwa ipo migogoro ya ardhi ambayo imetatuliwa na mingine imefikia hatua fulani hivyo itabidi nipitie mafaili ili nione naanzia wapi hivyo nitaifanyia kazi migogoro hiyo ila kwa sasa siwezi kusema sana”.ameeleza Fauzia.

Wananchi wa Kijiji cha Kwekinkwembe kata ya Mkindi tarafa ya Mswati Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, wametishia kurudisha kadi za uanachama wa CCM kwakuwa migogoro ya ardhi isiyotatuliwa kwa wakati.
Kutokana na hali hiyo wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan, kuingilia kati mgogoro wa ardhi kati ya Jamii ya Wakulima ya Wanguu na jamii ya wafugaji wa Kimasai.
Wananchi wametoa ombi hilo kwa Rais Samia, wakati wakizungumza na waandishi wa habari juu ya adha wanayokutana nayo kwa kufanyiwa uonevu na wafugaji wa jamii ya Kimasai.
Katika maelezo yao wanadai kuwa wamekuwa wakiishi maisha ya kukimbia kimbia huku na kule kutokana na kutishiwa na wafugaji hao.
Wamesema kuwa hata mashamba yao yapo hatarini kuchukuliwa.

Bakari Salimu Omari,Mkazi wa kijiji cha Kwekinkwembe ameeza kuwa jamii hiyo ya wakulima imeanza kumiliki mashamba hayo muda mrefu.
Akiendelea kutoa ufafanizi alieleza kuwa kuwa kijiji Kwekinkwembe kilianzishwa mwaka 1971 na ilipofia mwaka 1976 kilinzishwa Kijiji cha Mkindi na kuwekeana mipaka.
Omari ameeleza kuwa tatizo kubwa au ombi kubwa la wananchi ni kutaka viongozi kuhakikisha wanatatua mgogoro huo ikiwemo kuweka mipaka ya maeneo.
Naye Lukuwa Kabwanga chanzo chote cha migogoro ni kuingiliwa na jamii ya wafugaji ambao ni jamii ya kimasai.
Kwa upande wake Halima Kilo alieleza kuwa kitendo cha kuingiliwa kwenye mashamba yao na jamii ya wafugaji kinachangia kuwakosesha mapato hatua itakayosababisha washindwe kusomesha watoto wao.
Kwa upande wa Mtendaji wa Kata ya Mkindi aliyejitambilisha kwa jina moja la Makusudi alipotafutwa kuhusu mgogoro huo, alikiri kuwapo mgogoro wa siku nyingi na wanaendelea kusikiliza viongozi ili wapate mwongozo.
Mwisho.