Leo Mei 9 saa 7:30 usiku Uwanja wa Stadio Via del Mare utakuwa mwenyeji wa mchezo wa ligi kuu ya Serie A kati ya Lecce iliyopo nafasi ya 17 na Juventus waliopo nafasi ya 4.
Lecce wakiwa na pointi 32 wako hatarini kushuka daraja, wakitengwa na eneo la kushuka daraja kwa pointi 4 pekee. Juventus wana pointi 65, lakini wanashinikizwa na Roma na Como wanaokaribia kuwapokonya nafasi ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Juventus wanarekodi ya mechi 5 bila kushindwa, ikiwemo sare dhidi ya Hellas Verona na Milan, lakini ushindi mmoja tu katika mechi tatu za mwisho. Khephren Thuram ana shida ya goti na amekuwa akicheza chini ya uwezo, huku Kenan Yıldız akiwa na jeraha.
Upande wa Lecce, Lameck Banda ameanza kucheza tena baada ya jeraha na anaweza kuwa muhimu, huku wachezaji wengine kama Fofana, Gaspar na Sottil bado hawako tayari kikamilifu.
Katika historia ya makabiliano kati ya timu hizi, Juventus wana ubabe mkubwa wakiwa wameshinda mara 9 kwenye michezo 15 ya hivi karibuni, Lecce wakiwa na ushindi 1 pekee na sare 5. Mchezo wa mwisho kati yao Januari 2026 ulimalizika kwa sare ya 1-1, na katika mechi tatu za mwisho, Lecce wamefanikiwa kupata sare mara mbili. Hii inatoa matumaini kwa Lecce kwamba wanaweza kukwepa kichapo cha nyumbani.
Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Lecce wanatarajiwa kuanza na Walid Cheddira akiwa mshambuliaji mkuu huku Lameck Banda akitishia ubavuni. Juventus watakuja na mfumo wa 3-4-2-1, wakiwa na Jonathan David, Francisco Conceição na Kenan Yıldız wanaowaunga mkono washambuliaji. Ikiwa Thuram hatacheza, Weston McKennie anaweza kuchukua nafasi yake katikati akiwa na Manuel Locatelli, huku Emil Holm akiwa tayari kutokea ubavuni wa kulia.
Licha ya Juventus kuwa na ubora wa wachezaji na wanahitaji ushindi kwa ajili ya nafasi ya Champions League, Lecce nyumbani wanapigana kwa uhai wao kusalia Serie A. Juventus wameshinda mara moja tu katika mechi tatu za mwisho za ugenini, huku Lecce wakipata sare nyumbani na Fiorentina na kushinda ugenini dhidi ya Pisa.