MAHAKAMA Kuu, Masjala Ndogo ya Kigoma, imepanga kuanza kusikiliza kesi ya uchaguzi wa Jimbo la Kigoma Mjini katika hatua ya ushahidi kuanzia keshokutwa, Alhamisi 18 Juni 2026.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Hatua hiyo inatokana na kukamilika kwa taratibu za awali na za msingi za usikilizaji wa kesi hiyo, ambazo zimehitimishwa katika hatua ya usikilizwaji wa awali iliyofanyika jana Jumatatu 15 Juni 2026 jioni.
Katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Clayton Chipando, maarufu Baba Levo, alitangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi huo na hivyo kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Baba Levo alitangazwa kushinda kiti hicho akimzidi mpinzani wake mkubwa kutoka ACT-Wazalendo, mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Zitto Kabwe.